Habari Za Nyumbani–on jambonewspot.com

Visit www.jambonewspot.com…..your community website for more

Diaspora group working on Kenya presidential debates in the US

Posted by Administrator on January 30, 2012

The Kenya Diaspora Advisory council USA with the leadership of Kenya Diaspora Advisory council of New England is working on organizing presidential debates/town-hall meetings for all of the 2012 presidential candidates.

This will provide a forum for an independent political dialogue that will help the voters indetify leaders based on issues and not tribal affiliations.

The council will organize national debates/town-hall meetings that will see the candindates tour the USA and meet with kenyans in all the key states.
Advertisements

One Response to “Diaspora group working on Kenya presidential debates in the US”

 1. ITHAVETHI said

  Wazo nzuri lenye nia nzuri. Na kwa kweli mjadala kama huo mbele ya umma ni muhimu hasa wakati huu uchaguzi wa urais unaponukia. Lakini swali la kujiuliza ni hili: je, mbegu za ukabila zilizomea na kukomaa katika vichwa vya viongozi wa Kenya tangu tulipopata uhuru vitang’olewa kwa masaa matatu ya maswali kadhaa? La! Hebu chukua wakati huu kuwapekuapekua wagombezi wa kiti hicho kama Raila, Ruto, Peter Kenneth, Saitoti na wengineo.

  Viongozi hawa, kama wenzao bungeni, wamepawa kipawa cha kuongea maneno matamu matamu ijapo ni kutafuta kura. Ama tuseme kuwa wote wamefuzu katika vyuo vya kuongea kama cherehani au kasuku huku wakiwaahidi na kuwahadaa wananchi eti kwamba watatengeneza mabarabara, mashule, maabara, mahospitali, mabwawa, nishati, na kuboresha maisha yao punde tu watakapoingia bungeni.

  Kwa sababu ya kuhofia kutochaguliwa bungeni, basi wanatembelea wanganga ambao wanawashauri wafukuze “madoa doa” katika sehemu zao. Diposa unamuona Balala anachukua fimbo Mombasa, Raila, Anyang Nyong, Orengo, na viongozi wajaluo wenzao wanawavuruga Kisumu; Narok unamkuta Ole Ntimama, Ruto na wenzake wanashikilia chuki Eldoret, Burnt Forest, Ole Nguruine, Molo, Njoro, Kapenguria, Mlima Elgon, Londiani, Kedawa, Kericho, Bomet, Baringo na sehemu zingine katika Mkoa wa Bonde la Ufa. Baadhi ya “madoa doa” ya Wakenya kutoka makabila ya Wakikuyu, Wakamba, Wakisii, na wengineo.

  Swala kubwa ni hili, mbona Waturkana, Wamursi, Wamolo, Wanyagatom, Wasamburu, Wagabra, Wadaasanach, Wahamar Koke, Waborana, Warendille na wakenya wengine waishio Mikoa ya Kaskazini Mashariki na Kaskazini mwa Kenya hawawatimui mbio hao “madoa doa?”

  Ukwelo usemwe kwani ukweli upo. Itawachukua viongozi wa Kenya muda mrefu kukubali kuing’oa mbegu na mmea wa ukabila. Itawachukua Wakenya miaka nyingi kuacha kuhongwa na kuuza kura zao kwa shillingi mia moja, kuacha kuwachagua viongozi wao kwa misingi ya ukabila, na mwisho, kuwachagua wawapendao kulingana na maswala yanaowakabidhi. Utaweza kumshurutisha Mkikuyu ampigia kura Mturkana? Utaweza kumzungumzia Mjaluo kumpigia mwingine isipokuwa Raila. Na Mkalenjin je? Na Mluhya je? Na Mkamba je? Suluhisho? Wapeleke viongozi wote kuchukua shahada ya miaka minne katika shule na vyuo vya Tanzania ambako kabila yao ni moja tu: Utanzania!!!!!!

  Mijadala kama hio itakuwa tu kama kujipurisha marashi mwilini ingawa mwili watoa ufundo wa kupindukia makwapani.

Sorry, the comment form is closed at this time.

 
%d bloggers like this: