Habari Za Nyumbani–on jambonewspot.com

Visit www.jambonewspot.com…..your community website for more

The Day I will Never Forget: The tragedy of female circumcision

Posted by Administrator on February 26, 2012

Advertisements

2 Responses to “The Day I will Never Forget: The tragedy of female circumcision”

 1. ITHAVETHI. said

  Visa vya kuwafanyia tohara wasichana katika Mkoa wa Kaskazini mashariki mwa Kenya ni jambo la kawaida ambalo watumishi wa serikali wameshindwa kulimaliza. Ni mila ambayo imechimbia mizizi katika fikra na jinsia za watu wa makabila ya Wapokot, Waturkana, Wasamburu, Waborana, Wamursi, Warendille, na wengineo waishio katika Bonde La Ufa. Hasa ukeketaji huo wa wasichana wadogo hufanyika pale shule zinapofungwa, na ni jambo la kushangasha kuona kwamba wazee wa mitaa, ambao ndio hueneza na kulinda mila hio isififie, huonekana kila mara wakiandamana na machifu na manaibu wao katika baraza mle vijijini.

  Lakini kabila linalotumia njia mbovu katika ukekezaji wa wasichana wao ni Wapokoti na Wasamburu. Ingawa hakuna tohara inayoweza kusifiwa kwa njia yoyote, makabila ambayo yanajihusisha na vitendo na visa vya kuwatahirisha wasichana kwa minajiri ya kuwafanya wake wema katika siku za baadaye yatakiwa ipigwe marufuku mara moja. Hasira , nuksi, matusi, ukemewaji, laana, pingamizi, uadui na maneno makali ninayoyapata pale ninapojaribu kutokomeza mila hii kutoka kabila langu la linaniacha nikiwa mpweke kama kiumbe kisichokuwa na kwao.

  Mila hii, kwa hakika, imehimili pia katika makabila mengine kama ya wakisii, Wakikuyu, Wateso, Wakamba, Mijikenda na kadhalika. Ni tatizo ambalo litakuwa vigumu kulitokomeza kama katiba mpya inavyoagiza, kwa sababu viongozi waliochaguliwa na umma wanaogopa kupoteza kura pale wanapojaribu kulipinga katika mikutano ya hadhara. Jamii nyingi duniani pia hufuata mila hii hasa katika mataifa ya Kiafrika.

  Ukweli ni kwamba, ukeketaji huu wa wanawake ni kinyume cha maumbile na dharao kwa Mwenye Enzi. Tohara kwa wasichana wadogo wasiokuwa na hatia na fahamu kwa kinachoendelea, ni hatari kwa afya na maendeleo ya wanaokeketwa. Natumai kwamba viongozi wataochaguliwa katika majimbo wataiheshimu katiba mpya kwa kuelimisha umma adhari za kuiendeleza mila hii na kufungua ukurasa mpya wenye kuiheshimu jinsia za wanawake hasa madhara yanayowakumba warembo wetu.

 2. maggie said

  wat tradition is this,hurting kids these pple need to be hnaged or jailed

Sorry, the comment form is closed at this time.

 
%d bloggers like this: